ZINAZOVUMA:

Upinzani waunga mkono mapinduzi Gabon

Kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa aliyekuwa Rais wa...

Share na:

Hali ya utulivu wa kisiasa inaendelea kuimarika nchini Gabon toka kufanyike mapinduzi Agosti 30, 2023, na hii ni baada ya Kiongozi wa kijeshi, Jenerali Brice Nguema kukutana na Jean Ping, mpinzani na mkosoaji mkubwa wa Ali Bongo, Rais aliyepinduliwa madarakani.

Jean Ping na Rais wa mpito wa Gabon Brice Nguema walikutana ana kwa ana kwa mazungumzo ambayo yalimfanya Jean Ping, kuondoka huku akitabasamu.

Baada ya mkutano huo Jean Ping alisema, “Nimepewa heshima yangu kama mmoja wa watu muhimu katika nchi hii na nimefurahi kuwa na mazungumzo na kiongozi mpya”.

“Nafikiri kwamba Rais wa Jamhuri, Mheshimiwa Brice Oligui Nguema, amefanya kazi kubwa ya kusafisha nchi” aliongeza.

Kwa miaka saba iliyopita, Jean Ping ameishi katika kifungo cha nyumbani katika makazi yake katika eneo la Charbonnages huku akiendelea kudai ushindi wake katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 ambao anaamini kuwa aliibiwa na Ali Bongo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,