ZINAZOVUMA:

Upinzani nchini TOGO kugomea mabadiliko ya katiba

Wapinzani waingia mtaani kuwazindua wananchi juu ya mabadiliko ya katiba...

Share na:

Wabunge nchini Togo walizindua mashauriano ya kitaifa siku ya Jumatatu Aprili  08 kupinga mabadiliko ya katiba yaliyopitishwa na wabunge feki.

Mashauriano hayo yamekuja baada ya kuwa na mabadiliko ya kikatiba nchini humo, ambayo yalipitishwa na wabunge ambao uhalali wao wanaupinga.

Wabunge wa Togo watafanya ziara ya siku tatu kusikiliza na kuwafahamisha raia kuhusu mabadiliko ya katiba.

Watawala wa kimila na vikundi vilivyochaguliwa vinaripotiwa kuwa walengwa wakuu wa mashauriano hayo.

Katiba inayopendekezwa ambayo ilipitishwa Machi 25, inalipa bunge mamlaka ya kuchagua rais, na kufuta uchaguzi wa Rais nchini humo.

Hii inabadilisha mfumo wa serikali ya Togo kutoka serikali ya kirais hadi Serikali ya kibunge.

Badala ya muhula wa miaka 5 unaoweza kurejewa kwa sasa, mswada huo unapendekeza muhula mmoja kaka kikomo ya kipindi cha urais nchini humo.

Badala yake madaraka makubwa anakabidhiwa mtu anayefanana na waziri mkuu, atakayetambulika kama Rais wa baraza la mawaziri. Rais wa Baraza la mawaziri  atakuwa “kiongozi wa chama ambacho kinapata wabunge wengi katika uchanguzi”; au kiongozi wa muungano wa vyama utakaoshinda.

Hata hivyo upinzani wanahofia kuwa jukumu hilo linaweza kuwa njia ya Rais Gnassingbé kuendelea kushika madaraka nchini humo.

Historia ya hivi karibuni ya Togo imetawaliwa na ukoo wa Gnassingbé ambao umetawala tangu 1967.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya