Umoja wa Mataifa UN umetangaza kusitisha shughuli zote za kibinadamu nchini Niger. Hii inakuja baada ya wanajeshi nchini humo kutangaza kumpindua Rais mteule wa nchi hiyo.
Umoja wa mataifa umesema mpaka sasa zaidi ya watu milioni nne nchini humo kwa wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Katika hatua ya kuwaonya wanajeshi wa Niger, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa agizo la kuachiliwa mara moja na bila masharti yoyote kwa Rais wa Niger Mohamed Bazoum ambaye amezuiliwa na maafisa wa kijeshi.
Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema Rais Bazoum alizungumza na Rais Emmanuel Macron mapema leo hii na kumwambia kwamba yupo hai na ana afya njema tu.