ZINAZOVUMA:

Uhasama washika kasi nchi za Afrika Magharibi

Niger imewarudisha nyumbani mabalozi wake waliokuwa katika nchi za Ivory...

Share na:

Viongozi wa kijeshi nchini Niger, wamewarudisha nyumbani mabalozi wake waliokuwa katika nchi za Ivory Coast na Nigeria, baada ya matamshi ya Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, kuwa wanadiplomasia hao wanaunga mkono uvamizi wa kijeshi kwa nchi yao.

Rais Ouattara alikuwa amezungumzia kuhusu suala la kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kidemokrasia na kurudishwa madarakani kwa Mohamed Bazoum.

Pia alisema kuwa operesheni ya kijeshi kurejesha demokrasia nchini Niger inapaswa kuanza haraka iwezekanavyo ikiwa Niger tayari imekaidi agizo la ECOWAS.

Aidha Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imesisitiza kufanyika kwa mazunguzmo na kutatua changamoto zilizoko kwa njia ya kidiplomasia lakini inasema uingiliaji kati wa kijeshi bado uko mezani.

Hata hivyo umoja huo ulisema kuwa ulishangazwa na hatua kwamba viongozi hao wa mapinduzi wameamua kuendeleza mashtaka dhidi ya Bazoum kwa kile wanachosema ni uhaini mkubwa.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya