ZINAZOVUMA:

Uhaba wa wataalamu yawa kilio TCAA

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari amesema tatizo la uhaba...

Share na:

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA imesema moja ya changamoto kubwa inayokumbana nayo sekta ya Anga ni pamoja na kuwa na wataalamu wa kutosha, hali inayopelekea kulazimika kuajiri wataalamu wa kigeni kwa gharama kubwa zaidi.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari, katika maadhimisho ya 47 ya maonesho ya kibiashara ya saba saba.

“Kampuni zetu zinalazimika kuajiri marubani kutoka nje ya nchi ambao gharama zake ni kubwa zaidi” amesema.

Hata hivyo TCAA imetenga fungu kwa ajiri ya kuwapeleka marubani katika mafunzo ili kuongeza idadi ya wataalamu wetu, ambapo mpaka sasa kuna marubani 10 wanaoendelea na mafunzo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu amesema changamoto ya wataalamu inasababishwa na vijana kutokupenda kusoma masomo ya Sayansi na hata wanaoajiriwa wanakua na ufaulu mzuri lakini hawapo vzuri katika vitendo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya