ZINAZOVUMA:

Uganda: Waziri apigwa risasi na mlinzi wake

Waziri nchini Uganda amepigwa risasi na mlinzi wake kwa madai...

Share na:

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano ya Viwanda nchini Uganda, Mhe. Charles Okello Engola ameuawa kwa kupigwa risasi huko Kyanja na mlinzi wake aliyekuwa akimlinda.

Tukio hilo limetokea asubuhi hii ambapo imeripotiwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini ambapo ghafla Mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbilia Mtaani.

Majirani wamesema Mlinzi alisikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi na Waziri huyo. Mlinzi huyo baadaye aliingia Saluni moja iliyopo Jirani na nyumba ya Waziri kisha akawataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya