ZINAZOVUMA:

Uganda matatani mapenzi ya jinsia moja.

Uganda matatani baada ya kupitisha sheria dhidi ya mapenzi ya...

Share na:

Marekani imetishia kuiwekea vikwazo Uganda kama hawatabadili mawazo kuhusiana na muswada waliopitisha kuhusu mahusiano ya jinsia moja.

Aidha kwa upande mwingine pia umoja wa nchi za ulaya umeeleza wasiwasi wake kuhusu muswada huo wakisema kuwa ni kinyume cha Sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Ikumbukwe kuwa muswada huo uliwasilishwa na wabunge wa Bunge la uganda tarehe 10/3/2023 wakitaka watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuchukuliwa hatua.

Baada ya kupitishwa kwa muswada huo siku ya jana kumezuka taharuki kutoka kwa mataifa yanayounga mkono Mambo hayo na hata kufikia hatua ya Uganda kutishiwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya