Bondia wa Tanzania Twaha Kiduku amefanikiwa kuibuka na ushindi katika pambano lake lililofanyika usiku wa jana tarehe 22 Aprili, dhidi ya Iago Kiziria.
Ushindi wa Twaha Kiduku ulipatakana kwa “points” ambapo majaji wote watatu wamempa ushindi Kiduku kwa Pointi 98-92, 98-92, 97-93 licha ya mpinzani wake huyo ambaye ni raia wa Georgia kuonesha upinzani mkali.
Baada ya pambano hilo, Kiduku amesema mpinzani wake alikuwa mzuri na hiyo ilimlazimisha abadili staili ya upiganaji wake na ndio maana wamefika hadi Raundi ya 10.