ZINAZOVUMA:

TRA yafanya mabadiliko ulipaji kodi ya majengo

Mamlaka ya Mapato nchini TRA ikishirikiana na Shirika la Umeme...

Share na:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imetangaza mabadiliko ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya utozaji wa kodi ya majengo ambapo viwango vya utozaji vimebadilika pamoja na wigo wa ukusanyaji umeongezeka kwa kujumuisha nyumba zilizopo maeneo yote ya Wilaya.

Mamlaka imebainisha kuwa nyumba ya kawaida iliyokuwa inatozwa TZS 12,000 kwa mwaka, sasa itatozwa TZS 18,000 kwa mwaka sawa na shilingi 1,500 kwa mwezi.

Nyumba ya ghorofa katika maeneo ya Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji zilizokuwa zinatozwa TZS 60,000 kwa kila sakafu kwa mwaka, sasa zitatozwa TZS 90,000 sawa na TZS 7,500 kwa mwezi.

Vilevile, nyumba za ghorofa katika maeneo ya Halmashauri za Wilaya zilizokuwa zinatozwa TZS 60,000 kwa kila nyumba kwa mwaka, sasa zitatozwa TZS 90,000 kwa kila nyumba kwa mwaka sawa na TZS 7,500 kwa mwezi.

Aidha, mamlaka imesema utekelezaji huo unaanza mwezi Julai, 2023 na wamiliki wasiotumia umeme wa Tanesco wafike TRA kwa ajili ya kupatiwa ankara ya malipo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya