ZINAZOVUMA:

Tisa wafa Kenya kwa ugonjwa usiojulikana.

Ugonjwa usiojulikana umeibuka nchini Kenya na kuuwa tisa huku 80...

Share na:

Watu tisa wamefariki na wengine zaidi ya 80 kulazwa hospitalini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa usiojulikana katika kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya.

Msimamizi wa eneo hilo amesema kati ya watu tisa ambao wamekufa, sita walikuwa watu wazima na watoto watatu kati ya mwaka mmoja na mitatu.

Wengi wa watu walioathiriwa walionyesha dalili kama za mafua, macho ya manjano na maumivu makali ya kichwa, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti hivyo.

Mlipuko huo unajiri miezi miwili baada ya Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu nchini Kenya kugundua mbu washambuliaji katika maeneo ya Laisamis na Saku kaunti ya Marsabit.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya