ZINAZOVUMA:

Tinubu Mwenyekiti mpya ECOWAS

Umoja wa nchi za ukanda wa Afrika Magharibi umemchagua Raisi...

Share na:

Umoja wa Nchi za ukanda wa Afrika Magharibi ECOWAS umemchagua Raisi wa Nigeria kuwa Mwenyekiti wa umoja huo katika muda ambao nchi nyingi za ukanda wa Magharibi zikipitia machafuko.

Afrika ya Magharibi imeshuhudia mapinduzi ya kijeshi sita tangu mwaka 2020, hii ikionesha namna hali ya demokrasi ilivyoshuka katika ukanda huo na jeshi likishika hatamu.

Hata hivyo kulikua na jaribio la mapinduzi ya kijeshi hivi karibuni katika nchi ya Guinea Bissau ambapo Raisi wake Umaro Sissoco Embalo ndio alikua Mwenyekiti aliepita wa ECOWAS akimuachia nafasi Raisi wa Nigeria.

Raisi Tinubu amesema vipaumbele vyake katika ECOWAS ni kuhakikisha uimara na usalama wa siasa, amani pamoja na Ulinzi vitakua ndio nguzo katika kuongoza umoja huo wenye nchi 16.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya