Hivi karibuni Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Hussein Bashe alichapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter, kukataa Tanzania kuhusika na sakata la mbolea feki inayozagaa nchini Kenya.
Bashe alichapisha ujumbe huo baada ya mwanasheria wa Kenya Ahmednasir Abdullahi kuchapsha kuwa amepata fununu na ushahidi wa kutosha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa Tanzania.
“Tanzania haihusiki na sakata la mbolea feki, hivyo isihusishwe na sakata hilo” na kuongeza kuwa “Tanzania inafahamu ubora wa mbolea iliyozalishwa na viwanda vyake viwili na kuingizwa kenya kwa utaratibu unaotakiwa”
Taarifa ya mwansheria huyo inasema kuwa mbolea hiyo ilikuwa ni mchanganyiko wa Mchanga, mawe na kinyesi cha mbuzi. Na kusema kuwa ilitengenezwa na kuwekwa kwenye vifungashio nchini Tanzania.
Katika kupinga skendo hiyo Bashe alichapisha ujumbe unaosema kuwa Tanzania haihusiki na Kawaida ya Tanzania kufanya biashara kwa umakini na uaminifu.