ZINAZOVUMA:

Tanzania na Ufaransa mambo mazuri

Ushirikiano wa Tanzania na Ufaransa kibiashara wazidi kukua kufikia hadi...

Share na:

Ukuaji wa biashara kati ya Tanzania na Ufaransa umeongezeka kutoka kiasi cha Sh billioni 27.8 kwa mwaka 2015 hadi bilioni 94.5 kwa mwaka 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax amebainisha hayo alipofungua mkutano wa pili wa majadiliano ya kidiplomasia kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ufaransa uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mbali na kukua kwa biashara kati ya mataifa hayo mawili, pia kumekuwa na ongezeko la watalii kutoka Ufaransa ambapo kwa mwaka 2022 Tanzania ilipokea watalii 100,600 kutoka Ufaransa na kuwa nchi ya pili kuleta watalii nchini Tanzania.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,