ZINAZOVUMA:

Tafiti: “Energy drinks” zinaweza kuua.

Tafiti zinaonesha kuwa unywaji wa "energy drinks" kupita kiasi unaweza...

Share na:

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imesema katika utafiti waake mpya umebaini unywaji wa vinywaji vya kuongeza nguvu mwilini maarufu ‘energy drinks’ unaweza kuleta madhara kwenye mishipa ya moyo kuziba na hata kusababisha vifo vya ghafla.

Mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mafunzo JKCI na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Pedro Palangyo amesema utafiti huo unamhusisha kijana wa Kitanzania ambaye mshipa wake mkubwa wa moyo uliziba ghafla kwa asilimia 100, na vijana wengine wakipokelewa ambao wamekuwa wakipata changamoto mfanano na hiyo wakiwa na historia ya kutumia vinywaji hivyo.

Aidha, Dkt. Palangyo amesema kijana huyo hakuwa na visababishi vyote vitano hatarishi ambayo ni mgonjwa ya kuambukiza, hakuwa mtumiaji wa sigara na pombe, hakuwa na uzito mkubwa, ulaji wake ulikuwa wa kawaida na mwenye kuzingatia mazoezi. Kitu pekee kilichobainika ni mtumiaji wa ‘energy drinks’ ambapo alikuwa kitumia makopo mawili hadi matano kwa siku.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya