ZINAZOVUMA:

Syria na Saudia sasa mambo ni shwari

Raisi wa Syria ameonekana mi mwenye furaha na kukumbatiana na...

Share na:

Raisi wa Syria Bashar al-Assad alionekana ni mwenye furaha alipoingia katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Waarabu mjini Jeddah huku hatua hiyo ikionesha kwamba ameshinda vita vyake dhidi ya Syria.

Raisi huyo alikumbatiwa na Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman.

Ikumbukwe kuwa muongo mmoja uliopita, Wasaudi walifadhili waasi waliokuwa wanampinga Raisi Assad.

Sasa mtoto wa mfalme, anayejulikana kama Mohammed Bin Salman anataka kuunda upya Mashariki ya Kati, na anaihitaji Syria ndani yake.

Aidha Katika hotuba yake rais Assad alisisitiza kuwa Syria daima itakuwa mali ya ulimwengu wa kiarabu. Lakini nchi zingine hazipaswi kuingilia kati na kile kilichotokea ndani ya mipaka yake.

“Ni muhimu kuacha mambo ya ndani kwa wananchi wa nchi husika kwani wao ndio wenye uwezo wa kuyasimamia,” alisema.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,