ZINAZOVUMA:

SUKUK: CMA Kenya yaidhinisha SUKUK ya kwanza nchini humo

SUKUK ya bilioni 3 KES, ya kwanza Kenya na ya...

Share na:

Mamlaka ya soko mitaji nchini Kenya, laidhinisha hati fungani za kiislamu (Sukuk) za kwanza nchini humo.

Idhini hiyo ilitoka kwa ajili ya kampuni ye Linzi finco Trust, yenye thamani ya Shilingi bilioni 3 za Kenya.

Lengo la sukuk hiyo ni kufidia nakisi ya bajeti, katika ujenzi wa nyumba takriban elfu 3.

Hii ni hatua kubwa katika kupanua upatikanaji wa nyumba za bei rahisi, na zina athari ya moja kwa moja kwa raia ilisema taarifa kutoka CMA.

Utoaji wa huduma hii umerahisishwa kwa kurekebisha baadhi ya vipendele katika sharia ya fedha ya mwaka 2017 nchini humo.

Pia sheria nyingine nyingi ziliguswa na mabadliko haya makubwa zikiwemo sheria ya kodi ya mapato na Kodi ya ongezeko la thamani, ushuru wa stempu, sheria ya usimamizi wa fedha za umma na hata sheria ya vyama vya Ushirika pamoja na SACCO.

Lengo la mabadiliko hayo ya sheria, kutambua bidhaa mbalimbali za benki za kiislamu na kurahisisha utozaji kodi bidhaa hizo nchini humo.

Mbali na kurahisisha kampuni mbalimbali kupata mitaji, pia serikali ya Kenya imekuwa na lengo la muda mrefu la kujazia nakisi ya bajeti yake kwa kutumia Sukuk.

Huenda hatua hii ya Linzi kutoa Sukuk ya kwanza nchini humo, itasaidia kampuni nyingine na hata serikali ya Kenya kuchukua mfumo huo kujazia bajeti.

Hatua hii ya Kenya kubadili sheria zake nyingi ili kurahisisha mfumo wa fedha wa kiislamu, ni funzo kwa la kuigwa kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki zilizoanza kutumia mfumo wa fedha wa kiislamu.

Nchi nyingine ambayo imefanikiwa kuidhinisha Sukuk Afrika Mashariki, ni Tanzania ambayo iliidhinisha Sukuk ya KCB “FURSA SUKUK” Novemba 2022.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya