ZINAZOVUMA:

Sudan kusitisha mapigano

Pande mbili zinazopigana nchini Sudan zimekubaliana kusitisha mapigano kwa muda...

Share na:

Pande mbili zinazopigana nchini Sudan zimeafikiana kusitisha mapigano kwa muda baada ya mapigano hayo kuendela kwa wiki sita sasa.

Makubaliano ya awali ya jeshi na kikundi cha wanajeshi wa dharura -Rapid Support Forces (RSF) yamekuwa yakikiukwa katika kipindi cha dakika chache kabla ya utekelezaji wake kuanza.

Lakini mkataba mpya utaimarishwa na mpango wa ufuatiliaji wa kusitisha mapigano hayo utasimamiwa kulingana na taarifa ya Marekani na Saudi Arabia.

Kama sehemu ya siku saba za usitishaji huo wa mapigano wa kibinadamu , maafisa wa Sudan wamekubaliana kurejesha huduma muhimu.

Mapigano baina ya pande mbili yameliingiza taifa katika hali ya ghasia tangu yalipoanza mwezi uliopita, huku zaidi ya watu milioni wakiyakimbia makazi yao.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya