ZINAZOVUMA:

Spika Tulia ataka njia bora za kupambana na madhara ya Tabianchi

Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa...

Share na:

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ataka benki ya dunia kuruhusu njia bora zaidi za kusaidia maafa ya tabianchi kutumika.

Alisema hayo katika ufunguzi wa kikao cha kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi, yanayoikumba Dunia na utatuzi wake.

Mkutano wa jukwaa la kibunge wa huo uliofanyika tarehe 15 Aprili 2024 katika Makao Makuu ya Benki ya Dunia Washington DC nchini Marekani.

Dkt. Tulia amesisitiza umuhimu wa Benki ya Dunia na IMF kuruhusu njia bora zaidi kutumika ili kusaidia nchi zinazokumbwa na maafa ya mabadiliko ya tabianchi kupitia mfuko wa maafa.

Aidha, ameyaasa Mabunge kuwa chachu ya utekelezaji wa mkataba wa Mazingira wa Paris kwa vitendo zaidi kuliko majadiliano ili kukabiliana na madhara yanayotokea duniani.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya