ZINAZOVUMA:

Museven aijibu tena Benki ya Dunia

Raisi wa Uganda Yoweri Museven ameijibu tena Benki ya Dunia...

Share na:

Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa mara nyingine tena amekosoa uondoaji wa ufadhili wa Benki ya Dunia nchini kwake akisema kuwa shirika hilo linajidanganya ikiwa linadhani kwamba hatua hiyo itawatia hofu Waganda.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya X Museveni ameitaja Benki ya Dunia kama waigizaji wa kibebari wasio na akili na wasiojua kipi cha kuacha.

Wiki iliyopita, Benki ya Dunia ilisitisha ufadhili kwa Uganda kwa sababu ya sheria ya kupinga ushoga iliyopitishwa mwezi Mei, ambayo ilikinzana na maadili ya Benki ya Dunia.

Sheria hiyo imeibua ukosoaji kutoka kwa mashirika mbalimbali ya kimataifa kwa ukali wake, ikiwa ni pamoja na adhabu ya kifungo au kifo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya mahusiano ya jinsia moja.

Akijibu Benki ya Dunia wiki iliyopita Museveni aliishutumu kwa kujaribu kuishinikiza Uganda kubadili sheria kwa kusitisha ufadhili, lakini aliongeza kuwa Uganda itaendelea kujiendeleza hata bila msaada wa Benki ya Dunia.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya