ZINAZOVUMA:

Somalia: leta bidhaa yenye vyeti vya ubora

Katika kuhakikisha ubora wa bidhaa zinazoingia na zinazotoka nchini Somalia,...
Somali standards bureau logo and a mini world map showing location of Somalia
Somalia bureau of Standards logo

Share na:

Nchi ya Somalia imetaka waagizaji wa bidhaa mbalimbali kuwa na vyeti vya ithibati (certificate of conformity) kwa bidhaa wanazoingiza nchini humo.

Taarifa hiyo imetolewa na shirika la Viwango la Somalia (SOBS).

Taarifa hiyo imetaka waingizaji wa bidhaa na hata watoa bidhaa kwenda nje kuwa na vyeti hivyo ili kukidhi vigezo vya ubora vya kimataifa.

Shirika hilo pia limetaka mashirika na makampuni kama Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa, pamoja na makampuni ya kibiashara nchini humo kutopuuzia agizo hilo.

Inatarajiwa vyeti vya ithibati kuangalia kukaguliwa kuanzia tarehe 1 mwezi Septemba kulingana na maelezo ya SOBS.

Tayari mataifa mengine barani Afrika yamekuwa yakihitaji vyeti vya ithibati kwa bidhaa nyingi zinazoingia au kutoka katika mataifa hayo.

Hatua hii ya Somalia huenda ikafanya nchi ambazo hazijaanza utaratibu wa kuwa na vyeti vya ithibati kuchukua na kuanza nao ili kuongeza ubora wa bidhaa zinazokhja na zinazotoka Afrika.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya