ZINAZOVUMA:

Somalia kuwa mwanachama mpya EAC

Jumuiya ya Afrika Mashariki ipo katika majadiliano ya kuiidhinisha Somalia...

Share na:

Mazungumzo kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na Jamuhuri ya shirikisho la Somalia juu ya kuijumuisha Somalia katika umoja wa Afrika Mashariki yataanza kufanyika mapema kesho mjini Nairob, Kenya.

Taarifa hiyo ilitolewa mbele ya waandishi wa habari jumamosi mjini Arusha ambapo ndio yalipo makao makuu ya Jumuiya hiyo.

Mazungumzo ya kuijumuisha Somalia ndani ya EAC yalianza tangu mwezi wa pili mwaka huu katika kikao kulichowakutanisha viongozi wa nchi huko Burundi.

Katika kikao hicho ilitolewa ripoti juu ya kuidhinisha ujumuishwaji wa Somalia hata hivyo maamuzi hayakufikiwa kwa wakati huo na hivyo kusubiri kikao kingine ambacho kitafanyika kesho.

Kujumuishwa kwa Somalia ndani ya EAC kutafanya kuwe na nchi nane ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda na Somalia yenyewe.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya