ZINAZOVUMA:

“Sitashiriki mijadala ya Urais”

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hatoshiriki...

Share na:

Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kuwa hatashiriki mijadala ya urais ya chama cha Republican na wapinzani wake katika kinyang’anyiro cha kuwania Ikulu ya White House.

Rais huyo wa zamani alisema kura ya maoni ya hivi karibuni ilionyesha kuwa alikuwa na idadi ya kutosha kuwa maarufu mbele ya watu wengine wanaotarajiwa kuteuliwa kugombea urais na chama hicho katika uchaguzi wa 2024.

“Umma unanijua mimi ni nani na nilikuwa na ni Rais mwenye mafanikio,” aliandika kwenye kwenye mtandao wake wa kijamii.

Mjadala wa kwanza wa mchujo wa urais wa chama cha Republican unatarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti.

Kura za maoni za hivi karibuni zimeonyesha mara kwa mara kuwa Donald Trump ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya jinai kwa sasa kuwa ndiye anayeongoza miongoni mwa wagombea wengine wanaotarajiwa kuteuliwa na chama cha Republican, kugombea Urais.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya