ZINAZOVUMA:

Simba yashusha kifaa kutoka Rayon sports

Baada ya kukamilisha usajili sasa ni zamu ya kutambulishwa kwa...

Share na:

Baada ya kukamilisha usajili uongozi wa klabu ya soka ya Simba hii leo imeanza kutangaza wachezaji ambao wamewasajili kuelekea msimu mpya wa 2023/2024.

Mchezaji wa kwanza kutambulishwa ni kiungo mshambuliaji Willy Essomba Onana mwenye miaka 23 raia wa Cameron.

Onana amesajiliwa kutoka Rayon Sports ya Rwanda ambapo msimu uliopita aliibuka mchezaji bora wa ligi kuu nchini humo.

Onana amesaini ‘kandarasi’ ya miaka miwili kuwatumikia wababe hawa wa Tanzania.

Aidha wakati huo pia klabu ya soka ya Yanga Jana usiku imetangaza mchezaji wake wa kwanza ambae ni Mtanzania Nickson Kibabage akitokea klabu ya Singida Fountain Gate zamani ikifahimika kama Singida Big Stars.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya