Klabu ya Simba imeendelea na kutangaza wachezaji na benchi la ufundi ambalo watakua nalo katika msimu huu wa 2023/2024.
Hii leo saa saba katika muda waliotangaza wa kufanya utambulisho, wamemtambulisha kocha mpya wa makipa ambae watakua nae katika msimu huu.
Kocha huyo mpya anaitwa Daniel Cadena ambae sio mgeni katika mpira wa Tanzania kwani msimu uliopita wa 2022/2023 alikua akifanya kazi na klabu ya soka ya Azam.
Simba wamemtambulisha kocha huyo huku bado wakiwa hawajamtambulisha rasmi golikipa mpya ambae inasemekana anatokea Brazil na atatua nchini pamoja na kocha mkuu wa Simba.