ZINAZOVUMA:

Serikali yaomba ipewe muda kuhusu ATCL.

Serikali imeomba ipewe muda kufanyia kazi suala la kuimilikisha ndege...

Share na:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Simbachawene amesema serikali inaomba ipewe muda kufanyia kazi pendekezo la wabunge pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuimilikisha ndege shirika la ndege la Tanzania, ATCL.

ATCL imekuwa ikikodi ndege zake kutoka katika Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) jambo ambalo wadau wamedai kuiwa ni mzigo kwa Shirika la ndege kujiendesha kibiashara.

Katika ripoti hiyo ya ukaguzi kwa mwaka 2021/2022 iliyowasilishwa bungeni Alhamisi, Aprili 6, 2023, CAG licha ya kueleza kuwa shirika hilo limepata hasara kwa miaka mitano mfululizo, pia amebaini madudu katika uendeshaji wa ndege hizo.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya