ZINAZOVUMA:

Serikali yakubali sekta binafsi bandarini

Serikali nchini kupitia Waziri wake wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa...

Share na:

Serikali imesema ni lazima kushirikisha sekta binafsi kuendesha Bandari ya Dar es Salaam ili kukuza ufanisi.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema hayo bungeni Dodoma wakati anajibu hoja za wabunge waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Profesa Makame Mbarawa alisema mwekezaji huyo anapaswa kuwa na uwezo wa kuiwezesha bandari hiyo ifikie ufanisi wa viwango vya kimataifa ukiwamo wa mnyororo wa usafirishaji tangu mzigo unaingizwa kwenye meli hadi unafika kwa mteja.

“Kampuni hiyo lazima iwe na mtandao mpana kupata mizigo kwenye masoko ya usafirishaji maji duniani, iwe kampuni kubwa ya kimataifa inayojulikana duniani na wawe na uwezo wa kimataifa kuendesha na kuendeleza shughuli za bandari,” alisema Profesa Mbarawa.

Aidha profesa Mbarawa aliwaeleza wabunge kuwa kampuni yenye sifa hizo itakapopatikana itapunguza muda wa meli kushusha mizigo kutoka siku tano hadi saa 24, kuongeza meli zinazokuja Bandari ya Dar es Salaam na itapunguza muda kushusha makasha kutoka siku nne hadi siku moja na nusu.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya