ZINAZOVUMA:

Serikali imefuta chama cha upinzani, Senegal

Serikali nchini Senegal imekifuta chama cha mwanasiasa maarufu na mpinzani...

Share na:

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko ambae alikua akishtakiwa kwa kuongoza uasi na kushikiliwa na jeshi la polisi, chama chake kimefutwa na serikali nchini humo.

Mapambano baina ya waandamanaji na polisi yalishamiri baada ya hatua hiyo iliyofanywa na serikali.

Sonko ambae ni mgombea wa urais na mkosoaji mkubwa wa Rais Macky Sall amekuwa akikabiliwa na msururu wa kesi ambazo anadai zina lengo la kumdhoofisha kwenye uwanja wa siasa.

Siku ya Ijumaa, alikamatwa kwa tuhuma mpya zinazohusiana na maoni aliyotoa katika mikutano ya hadhara aliyofanya na makosa mengine tangu mwaka wa 2021.

Aidha baada ya kufunguliwa mashtaka, Waziri wa Mambo ya Ndani alitangaza kwamba chama cha Sonko cha PASTEF kitafungiwa kwa kuchochea uasi na kusababisha uharibifu na vifo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya