ZINAZOVUMA:

Senegal inataka amani.

Viongozi nchini Senegal wameshauriana na kuamua kusitisha maandamano yaliyotarajiwa kufanyika...

Share na:

Chama cha upinzani nchini Senegal kimeahirisha maandamano yake yaliyopangwa kufanyika hii leo tarehe 3 mwezi Aprili.

Viongozi wa chama hicho wametoa tamko hilo baada ya kushauriana na viongozi mbalimbali wa vyombo vya usalama nchini humo.

Lengo la maandamano hayo yalikua ni kumuunga mkono kiongozi wao chama cha Pastef Party Ousmane Sonko aliyepelekwa mahakamani kwa shitaka la kumkashifu waziri wa utalii nchini Senegal.

Mbali na taarifa hiyo ya kuahirisha maandamano hayo kutoka kwa waandaaji, Mji Mkuu wa Dakar nchini Senegal umezuia maandamano hayo kufanyika katika mji huo kuepusha fujo na kuvunjika kwa amani.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya