ZINAZOVUMA:

Sancho aondolewa kikosini mpaka atakapo omba msamaha

Kocha wa Manchester United amempa adhabu Jadon Sancho ya kufanya...

Share na:

Mchezaji wa klabu ya Manchester United Jadon Sancho amezuiliwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake mpaka pale atakapomuomba radhi kocha wa timu hiyo.

Imebainishwa kuwa winga huyo amepewa zuio la kufanya na wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Manchester United hadi pale atakapomaliza tofauti zake na mwalimu wake, Erik ten Hag.

Sancho ametakiwa kufanya mazoezi na wachezaji wa timu ya vijana cha ya Manchester United kwenye Uwanja wa Carrington ikiwa ni adhabu kutoka kwa kocha.

Kosa la Sancho ni baada ya kumkosoa Ten Hag na kumuita muongo baada ya kocha kusema kuwa hakumpanga Sancho katika mchezo dhidi ya Arsenal kwa kuwa hakuonesha kiwango kizuri mazoezini.

Sancho alisema haelewi kwanini hakupangwa kwenye kikosi lakini sio kweli kuwa hakuonesha kiwango kizuri mazoezini hivyo kocha wake alidanganya.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya