ZINAZOVUMA:

Sababu za Rais wa China kutohudhuria mkutano wa G20

Mgogoro kati ya India na China watajwa kuwa sababu ya...

Share na:

Taarifa kutoka nchini China zimesema kuwa Rais Xi Jinping huenda hatashiriki mkutano unaozikutanisha nchi 20 tajiri duniani (G20) utakaofanyika kuanzia wiki ijayo.

Taarifa zimesema kuwa mgogoro kati ya China na India ndio sababu, hivyo ni ngumu Kwa Rais Xi Jinping kuhudhuria kwakua India ndio mwenyeji wa mkutano huo.

Kutojuhudhuria kwa Rais Xi Jinping kutafanya uwezekano wa kukutana na mpinzani wake kiuchuni Rais wa Marekani, Joe Biden kuwa mdogo.

Taarifa zinasema China itawakilishwa na Waziri Mkuu wake, Li Qiang huko jijini New Delhi kuanzia Septemba 9 hadi 10 mwaka huu.

Rais Xi mara ya mwisho alikutana na Biden katika mkutano wa kilele wa G20 huko Bali, Indonesia Novemba mwaka jana.

Hata hivyo Rais wa Marekani Joe Biden angetamani Rais Xi Jinping ahudhurie mkutano huo kama alivyosema kwenye mahojiano yake kuwa “Natumai atahudhuria,”

Rais wa Urusi Vladimir Putin tayari amesema hatohudhuria kwenda New Delhi na badala yake atamtuma Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov kwenda kumuwakilisha.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya