ZINAZOVUMA:

Ruto atoa sharti kwa Odinga

Raisi wa Kenya William Ruto amesema yupo tayari kukutana na...

Share na:

Rais wa Kenya, William Ruto ametoa sharti kwa Kiongozi wa upinzani Raila Odinga kabla ya kufanya mazungumzo kuwa kusiwepo na maandamano tena nchini humo.

Ruto amesema yupo tayari kukutana na Raila Odinga, na yuko tayari kutoa ustahimilivu katika masuala ambayo yatasaidia maendeleo ya taifa.

Ametoa kauli hiyo wakati wa ibada ya kanisa Kaunti ya Kwale siku ya Jumapili, ambapo amesema atakutana na kiongozi wa upinzani na timu yake wiki hii.

Hata hivyo, Ruto ametoa sharti hilo kwa upinzani kabla ya mazungumzo ambayo yatasimamiwa na aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olusegun Obasanjo ambapo amesema kwamba hakuna kiongozi yeyote atakayepanga maandamano ya vurugu nchini tena.

“Nilizungumza na kiongozi wa upinzani Raila na timu yake, nikawaambia kuwa sisi ni nchi ya kidemokrasia inayofuata katiba na sheria. Tunaweza kutokubaliana katika masuala mengi lakini hakuna kiongozi wa sasa, wa zamani au wa baadaye atakayepanga vurugu au uharibifu wa mali. Hilo halitatokea tena Kenya,” amesema.

Ameongeza kuwa “Tumeafikiana kuwa vurugu na uharibifu wa mali hautakuwa sehemu ya siasa na utawala wa Kenya. Mambo mengine tunaweza kuzungumza,” aliongeza.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya