ZINAZOVUMA:

Ruto aingia kwenye mkutano na gari ya umeme

Raisi wa Kenya William Ruto ameonesha jinsi anavyothamini ubunifu na...

Share na:

Rais wa Kenya, William Ruto, ameonyesha uongozi wa kipekee katika kusaidia ukuaji wa Teknolojia na Nishati ya umeme Kwa kutumia gari ya umeme kama sehemu ya msafara wake kwenye mkutano wa mabadiliko ya Hali ya Hewa uliowakutanisha viongozi wa Afrika huko Nairobi.

Raisi Ruto aliendesha mwenyewe gari la umeme kutoka Ikulu ‘State House’ kwenda kwenye eneo la mkutano.

Gari hilo la umeme ni aina ya ‘Autopax Air EV Yetu’ ambalo limetokana na ubunifu wa ndani na limetengenezwa Nairobi.

Gari la ‘Autopax Air EV Yetu’ ni matokeo ya ushirikiano kati ya SAIC–GM–Wuling na Kenya na itasaidia kukuza uingizaji wa magari ya umeme nchini Kenya.

Rais Ruto amekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono ukuaji wa Teknolojia na ameonyesha mfano mzuri kwa viongozi wengine.

Aidha serikali yake imechukua hatua za kuharakisha uingizaji wa pikipiki za umeme, baiskeli za umeme, na mabasi ya umeme kama sehemu ya mpango wa kufikia nishati safi kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya