ZINAZOVUMA:

Rita wataja sifa za wosia kisheria

Ofisi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini Rita wametoa...

Share na:

Ofisi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umetaja sifa sita za wosia halali kupitia kwa Ofisa wake wa Sheria, Janeth Mandawa ambae amesema wosia ni tamko analolitoa mtu mwenye akili timamu akieleza namna ya kugawa mali zake kwa warithi wake.

Mandawa amesema mhusika anapaswa kutoa tamko hilo bila shinikizo, vitisho, ushawishi au kurubuniwa.

Alisema wosia lazima uwe umeandikwa kwa kalamu isiyofutika, uwe umetaja mali, umetaja warithi ni akina nani na lazima ueleze mgawanyo wa mali za mhusika.

“Wosia lazima ubatilishe wosia mwingine wowote uliowahi kutolewa kwa njia ya mdomo ama kwa njia ya maandishi, na wosia lazima uwe na tarehe na uwekwe sahihi,” alisema Mandawa.

Aliongeza: “Mtoa wosia anaweza akamtaja msimamizi wa mirathi yake, lakini pia anapata nafasi ya kueleza angependa kuzikwa wapi.”

Alisema wosia unapaswa kurithisha warithi wote halali ambao wangestahili kurithi hata kama kusingekuwa na wosia, lakini usipozingatia hilo unakaribisha pingamizi unapopelekwa mahakamani kuthibitishwa.

Alisema anayeandika wosia lazima azingatie kuwa anachokirithisha ni mali yake na haruhusiwi kuwanyima warithi halali isipokuwa kama atathibitisha kuwa mrithi husika aliwahi kujaribu kuua.

“Wosia unaelekeza kurithisha mali kwa watu ambao kama kungelikuwa hakuna wosia basi wao ni warithi kwa sheria ambayo inasimama kurithisha kwa staili ya maisha ambayo huyu mtoa wosia ameishi,” alisema.

Alifafanua: “Warithi wa kwanza lazima wawe warithi halali, lakini wosia pia unaweza kumrithisha mtu yeyote ambaye mtoa wosia atapenda kumrithisha. Tumekuwa mashahidi tumeona watu wakirithisha mali zao kwa taasisi, wanaweka wakfu, wanatoa zawadi.”

Alisema sheria ya kuandaa na kuhifadhi wosia inaruhusu kufanya mabadiliko ya wosia kila mtoa wosia anapopenda kufanya mabadiliko au kama shahidi wake ameaga dunia hivyo atamweka shahidi mwingine ili wosia wake usipoteze sifa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya