ZINAZOVUMA:

Ripoti ya CAG Zanzibar kuleta mazito

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Raisi wa serikali ya...

Share na:

Raisi wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi amesema hayupo tayari kuwalinda wabadhirifu wa mali za umma.

Ameahidi Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/2022 itasomwa hadharani Jumamosi na watakaohusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Unguja alisema huo ndio msimamo wake na yeye ndiye aliyeanzisha utaratibu wa kusomwa kwa ripoti hiyo hadharani mara alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Alisema amefanya hivyo kwa ajili ya kuweka wazi utendaji wa watumishi wa umma waliokabidhiwa majukumu ya utendaji ambapo lengo ni kujenga utawala bora na nidhamu ya fedha za umma.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya