ZINAZOVUMA:

Ramaphosa asisitiza msimamo wake

Raisi wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza kuwa nchi yake...

Share na:

Raisi wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake itaendelea kupinga wito wa kuachana na sera yake huru ya mambo ya nje na isiyofungamana na upande wowote.

Akizungumza siku ya Alhamisi kwenye sherehe za Siku ya Afrika huko Krugersdorp, magharibi mwa Johannesburg, Ramaphosa alisema bara la Afrika mara nyingi linaingizwa kwenye migogoro nje ya mipaka yake.

“Afŕika Kusini haijaingizwa na haitaingizwa katika mashindano kati ya mataifa yenye nguvu duniani.

Tutadumisha msimamo wetu kuhusu utatuzi wa amani wa migogoro popote pale migogoro hiyo inapotokea,” Raisi Ramaphosa alisema.

Uhusiano wa Afrika Kusini na Marekani umekuwa mbaya tangu Afrika Kusini ilipochukua msimamo usiofungamana na upande wowote katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Hili lilichochewa zaidi na matamshi ya hadharani ya hivi karibuni ya yaliyotolewa na balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Reuben Brigety, kwamba nchi hiyo ilikuwa imeiuzia Urusi silaha.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya