ZINAZOVUMA:

Rais wa Burundi akanusha kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi

Raisi wa Burundi akanusha upotoshaji wa jaribio la kumpinduliwa wakati...

Share na:

Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye amekanusha madai ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi kwenye taifa lake wakati akiwa nje ya nchi kwa kipindi cha wiki mbili.

Rais Ndayishimiye alikua nchini Cuba kwa ziara kikazi na baada ya hapo kuelekea Marekani ambako alihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New York.

Siku moja baada ya kiongozi huyo kuondoka nchini kwake tarehe 10 ya mwezi Septemba 2023, taarifa ziliaanza kusambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwepo kwa njama za kutekeleza mapinduzi dhidi yake.

Katika hotuba yake baada ya kurejea jijini Bujumbura usiku wa Jumapili, Rais Ndayishimiye alihusisha taarifa hizo za kupinduliwa kwa serikali yake na watu ambao walikuwa wanataka kuharibu sifa ya taifa la Burundi.

Hata hivyo mpaka hivi sasa aliesambaza taarifa hizo za upotoshaji bado hajafahamika.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya