ZINAZOVUMA:

Rais Traore aijibu Ufaransa

Raisi wa Burkina Faso Ibrahim Traore amesema kuwa misaada ya...

Share na:

Raisi wa Burkina Faso Ibrahim Traore amesema kuwa misaada ya Ufaransa kwa miaka 63 haijawahi kuwa na faida yoyote katika Taifa hilo.

“Tumekuwa tukipokea misaada ya Ufaransa kwa miaka 63, lakini nchi yetu haijaendelea, hivyo kuikata kutoka kwetu sasa hakutatuua, badala yake kutatuhamasisha kufanya kazi na kujitegemea wenyewe.”

Maneno hayo ya Traore yamekuja baada ya Ufaransa kutangaza kusitisha misaada Burkina Faso pamoja na Mali baada ya nchi hizo kuonekana kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi nchini Niger.

Traore ambaye anatajwa kuwa Rais mdogo kuliko wote ulimwenguni, aliingia madarakani mwaka jana akiwa na umri wa miaka 34.

Alimpindua mwenzake, Paul-Henri Sandaogo Damiba ambaye pia aliingia madarakani kwa mapinduzi na kuongoza kwa kipindi cha Januari 2022 hadi Septemba 2022.


Aidha Ibrahim Traore anaamini nchi zinazoongozwa kijeshi ndio zina utawala bora na anahitaji zisiingiliwe na shinikizo za kimataifa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya