ZINAZOVUMA:

Rais Samia ziarani nchini Korea kusini

Rais Samia atakuwa kwenye ziara ya siku 7 Korea Kusini...

Share na:

Rais Samia anatarajiwa kuanza ziara ya siku 6 nchini Korea Kusini, kuanzia Mei 30 baada ya kupata mwaliko rasmi kutka kwa Rais wa Taifa hilo la Asia.

Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ya Rais Samia itakuwa na sehemu kuu mbili, Ya kwanza ni ziara rasmi ya kiserikali ya Tanzania nchini Korea Kusini, nay a pili ni Rais samia kuhudhurria mkutano wa Mkuu wa nchi za AFrika na Korea.

Mkutano Mkuu wa nchi za Afrika na Korea Kusini, unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 03 na 04 mwezi juni baada ya kumalizika Ziara ya Rais Samia.

Rais Samia atapata nafasi ya kuhutubia na kuzungumza katika jopo moja kati ya manne yaliyoandaliwa katika mkutano huo.

Serikali inatarajiwa kuingia mikataba saba na Seriali ya Korea Kusini, ukiwamo mmoja wa kupokea msada kwa njia ya mkopo nafuu wa wa Dola za marekani Bilioni 2.5.

“Makubaliano hayo ya ushirikiano wa kimaendele baina ya mataifa yetu ni mapya, na Mkataba mkubwa kati ya mikataba hii saba ni mkataba wa mkopo utakao kwenda kuboresha sekta za Elimu, Afya na miundombinu nchini” alisema Waziri Makamba.

Mikataba mingine itakayosainiwa ni ushirikiano katika maendeleo ya uchumi wa buluu, kutambua vyeti ya mabaharia, tamko la pamoja la uanzishwaji wa majadiliano na mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi.

Pia Serikali inatarajiwa kuingia makubaliano ya kushirikiana kati ya Taasisi ya Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Taasisi ya Sayansi na Miamba na Madini ya Korea, kwenye utafiti, uchoraji ramani, rasilimali na shughuli za maabara.

Hati nyingine ya makubaliano ni kati ya Wizara ya Madini ya Tanzania na Wizara ya Viwanda na Biashara ya Korea, kwenye kuchambua na kufanya utafiti wa madini mkakati.

Na kuongezea kuwa itasainiwa Hati ya mkataba wa makubaliano kati ya Shirika la Taifa la Madini (Stamico) na Shirika la Ukarabati wa Migodi na Rasilimali za Madini la Korea Kusini.

Ziara hiyo pia inatarajiwa kuzalisha ushirikiano wa Tanzania na Korea Kusini kweye Sekta ya Anga, kupitia Chuo Kikuu cha Usafiri wa Anga cha Korea, ili kuboresha usafiri wa anga nchini, namna ya kuendesha sekta hiyo kibiashara, pamoaja na huduma mbalimbali, tafiti na uratibu wa viwanja vya ndege.

Chuo hicho cha masuala ya Anga nchini Korea Kusini, kitamtunuku Rais Samia Shahada ya Heshima ya Udaktari katka menejimenti ya Usafiri wa Anga.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya