ZINAZOVUMA:

Rais Samia: Mtwara ndio bandari ya korosho

Rais Samia ataka korosho zote zipitie bandari ya mtwara baada...
Mtwara Port after expansion
Mtwara Port after expansion

Share na:

Rais Samia ametoa maagizo ya korosho zote za kusini zisafirishwe kwa Bandari ya Mtwara.

Mama Samia ameyasema hayo katika ziara yake mkoani Mtwara, na kuongeza kuwa anayetaka kusafirisha kwa bandari nyingine aombe kibali kwa Mkuu wa Mkoa.

Hatua hii itapunguza usafirishaji wa korosho kwa kutumia barabara hadi Mkoani dar es Salaam.

Maagizo haya yanahusu Zaidi korosho ghafi zinazotarajiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Mama Samia amesema hayo ili uwekezaji uliowekwa katika bandari ya Mtwara uwe na Tija.

Serikali imewekeza zaidi ya Bilioni 47 kukarabati bandari ya Mtwara, ili uongeza ufanisi bandarini hapo.

Mbali na maelekezo hayo ya kusafirisha korosho kwa bandari ya Mtwara, Rais Samia ametaka mamlaka zinazohudumia zao hilo kujadili na wadau juu ya changamoto za zao hilo.

Waziri Mbarawa alisema kuwa bandari hiyo imeongeza kiwango chake kutoka tani laki 5.92 hadi Tani milioni 1.63 kwa mwaka.

Na kuongeza kuwa bandari hiyo imeanza kushusha na kupakia Kontena na imeshapitisha kontena elfu 51 kwa mwaka wa fedha uliopita.

Kwa sasa bandari ya Mtwara ni ya pili kwa ubora, baada ya Bandari ya dar es Salaam.

Serikali ya Awamu ya sita ina mpango wa kutengeneza bandari maalum kwa ajili ya kushughulikia bidhaa kama Saruji, mbolea na makaa ya mawe kutoka kanda ya kusini.

Ili kufanikisha mpango huo, serikali imeandaa mpango wa kujenga bandari maeneo ya Mgao, inayotarajiwa kugharimu bilioni 150 za Tanzania.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya