ZINAZOVUMA:

Rais Ruto yupo tayari kuzungumza na Odinga

Raisi wa Kenya William Ruto amesema yupo tayari wakati wowote...

Share na:

Rais wa Kenya William Ruto amesema yuko tayari wakati wowote kukutana ana kwa ana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Hii inakuja baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali ambayo yamezua taharuki ndani ya nchi hiyo na kimataifa.

Raisi Ruto aliandika hayo kwenye mtandao mtandao wake wa twitter akieleza kuwa baada ya kurudi kutoka Tanzania kwenye mkutano wa viongozi wa Afrika basi atakuwa tayari kuzungumza na Raila Odinga.

Kauli hiyo ya Rais Ruto imekuja baada ya Raila Odinga kumshutumu kwa kutohudhuria mkutano wa kwanza ambao uliandaliwa kwa lengo la kutafuta suluhu.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya