ZINAZOVUMA:

Rais Edgar Lungu: Nipo katika kifungo cha nyumbani

Aliyekuwa Rais wa Zambia wa zamani Edgar Lungu asema yupo...

Share na:

Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, ametoa msisitio kuwa kwa jinsi anayoishi sasa “yupo katika kifungo cha nyumbani”, huku polisi wakisema kuwa wanamfuatilia na kumlinda kwa “kwa usalama wake tu”.

“Siwezi kutoka nje ya nyumba yangu bila kukabiliwa na polisi ambao hunirudisha ndani,” alisema Lungu akizungumza na BBC.

Ijumaa iliyopita, Bw. Lungu aliambia BBC kwamba amezuiliwa kwenda kwenye uchunguzi wa matibabu na kuacha jogging ya asubuhi baada ya polisi kumwambia hawezi kutoka nyumbani.

Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu akizungumza jambo na wananchi baada ya mazoezi ya kukimbia

Mbali na malalamiko hayo pia alisema kuwa aliwahi kutolewa kwenye ndege ambapo alikuwa na akihudhuria mkutano, ikabidi aahirishe safari hiyo.

Na kuongeza kwa kusema “Nakabiliana na matokeo ya kurejea kwenye siasa na niko tayari kwa hilo”.

Edgar Lungu ametangaza kurudi kwenye siasa mwezi oktoba mwaka jana, na tangazo hilo lilisababisha serikali kufuta mafao yake ya kustaafu.

Hii ni baada ya kutangaza kustaafu siasa, pale aliposhindwa na mpinzani wake Hakainde Hichilema katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021.

Pia alisema kuwa polisi walikuwa chini ya maagizo ya “kunivizia usiku, kuniteka, kunidhalilisha, na kunikamata kwa nguvu kama mhalifu sugu”.

Katika kuelezea sintofahamu hiyo ya kumfuatilia Kiongozi huyo wa zamani, Mkuu wa polisi Raphel Musamba Alhamisi alisema ni utaratibu wa kawaida kufuatilia harakati za kiongozi wa zamani “kwa usalama wake tu”.

Na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi hawana njama za kumvamia na kumdhalilisha kiongozi huyo.

Katika kuelezea sakata hilo Msemaji wa Ikulu Clayson Hamasaka alikanusha madai ya Bw. Lungu, na kusema kuwa akisema kiongozi huyo wa zamani alikuwa “akipita kwa uhuru katika miji yetu, akitekeleza haki zake za uhuru wa kusema na kujumuika, uhuru ambao aliwanyima wengine wakati mmoja”.

“Hivi sasa, Bw. Edgar Lungu ni mwanasiasa wa upinzani mwenye nguvu nchini Zambia. Sheria za nchi zinaeleza wazi matarajio kwa kiongozi wa upinzani,” alisema Bw. Hamasaka katika taarifa yake.

Akiwa kwenye ibada ya kanisa Jumapili iliyopita, Bw. Lungu alionya juu ya mabadiliko ya utawala kabla ya uchaguzi ujao, akisema “mtoto anaweza kuzaliwa kabla ya miezi tisa”.

Kauli ambayo Mkuu wa polisi alisema kuwa watamuita Bw. Lungu kuelezea juu kauli yake hiyo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya