ZINAZOVUMA:

Rais aliyepinduliwa kufunguliwa mashatka Niger

Jeshi nchini Niger limetangaza kumfungulia kesi Rais Mohamed Bazoum kumtuhumu...

Share na:

Jeshi la Niger limesema litamfungulia mashitaka ya uhaini Rais Mohamed Bazoum (63), aliyeondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi.

Hatua hiyo inakuja saa chache baada ya kundi la wanazuoni waandamizi wa Kiislamu kusema viongozi wa mapinduzi ya nchi hiyo wako tayari kwa diplomasia kutatua mzozo wao na jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi (ECOWAS).

Katika taarifa yake iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, msemaji wa jeshi la Niger, Kanali Amadou Abdramane ametaja mashtaka dhidi ya Bazoum kama uhaini ambao unahatarisha usalama wa ndani na nje ya nchi nchi hiyo.

Aidha, Kanali Abdramane ameondoa wasiwasi kuhusu afya ya Bazoum kudhoofika na kueleza kuwa kiongozi huyo alionana na dakatari kwa ajili ya kupima afya yake siku chache zilizopita.

“Daktari hakutoa ripoti ya matatizo yoyote kuhusu hali ya afya ya rais aliyeondolewa madarakani na wanafamilia wake,” amesema.

Bazoum na familia yake wamezuiliwa katika makazi rasmi ya Rais huko Niamey tangu mapinduzi yaliyofanyika Julai 26 huku ECOWAS ikitoa wito wa kurejeshwa madarakani kwa kiongozi huyo na kuiwekea Niger vikwazo vikali vya kiuchumi pamoja na kutishia kuingilia kijeshi ikiwa utawala wa kiraia hautarejeshwa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya