ZINAZOVUMA:

Qatar yawahukumu kifo wahindi nane

Mahakama nchini Qatar imewahukumu kifo wastaafu nane wa jeshi la...

Share na:

Mahakama ya Qatar imewahukumu watu nane kifo, kwa makosa yanayotazamiwa kuwa ni ujasusi wa teknoljia ya kijeshi.

Watu hao raia wa India na ni wanamaji wastaafu wa india, waliajiriwa katika kampuni ya Al Dahra Global nchini Qatar.

Wanamaji hao kutoka India waliohukumiwa kifo ni Kapteni Navtej Singh Gill, Kapteni Birendra Kumar Verma, Kapteni Saurabh Vasisht, Kamanda Amit Nagpal, Kamanda Purnendu Tiwari, Kamanda Sugunakar Pakala, Kamanda Sanjeev Gupta na Baharia Ragesh

Na vyanzo vinasema kuwa kampuni hiyo na maafisa hao wa India wa zamani, walikuwa wakisimamia uingizwaji wa manowari ndogo toka Italia.

Pamoja na wahindi hao pia kuna Raia wa Qatar wawili ambao hawakutajwa majina, na raia wa Oman Khamis Al Ajmi, ambaye pia alikuwa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Dahra Global.

Hata hivyo hakuna taarifa za kuachiwa kwa raia wa Qatar, ila kuna taarifa Al Ajmi aliachiwa mwezi Novemba 2022 kabla ya kuanza Kombe la Dunia.

Serikali ya India imekuwa karibu na watu hao nane pamoja na familia zao, na imekuwa ikiangalia namna bora ya kuweza kuachiliwa.

Hata hivyo serikali na viongozi mbalimbali walishtuka mno baada ya kusikia hukumu iliyotolewa juu ya wanamaji hao.

Mbunge wa chama cha Congress ameitaka serikali ya India kufanya kila linalowezekana, ili wanamaji hao wachiwe.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya