ZINAZOVUMA:

Putin ateta na Mwana Mfalme wa Saudi Arabia.

Raisi wa Urusi Vladimir Putin amefanya mazungumzo na Mwana Mfalme...

Share na:

Raisi wa Urusi Vladimir Putin amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mwana Mfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman Al Saud, na kujadili kuhusu migogoro inayoendelea mashariki ya kati.

Mazungumzo hayo yalifanyika mara baada ya waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan kutembelea Syria kwa mara ya kwanza na kujionea hali iliyopo huko.

Putin na Mwana Mfalme pia wamezungumza kuhusiana na mahusiano ya kibiashara baina ya mataifa hayo mawili ili kukuza uchumi wa nchi zao.

Aidha Putin amegusia suala la Saudi Arabia kushirikiana na umoja wa nchi za BRICS ambao unaundwa na Brazil, Urusi, India, China, pamoja na Afrika kusini.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya