ZINAZOVUMA:

Putin aahidi kutuma nafaka bure kwenda Afrika

Raisi wa Urusi Vladimir Putin amesema atatuma nafaka kwenda kwa...

Share na:

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameeleza kwamba nchi yake itatuma nafaka kwenda katika mataifa sita ya Afrika bila malipo.

Putin ameyasema hayo katika mkutano unaofanyika kati ya Urusi na nchi za Afrika mjini St Petersburg, na kuweka wazi kuwa katika miezi michache ijayo wataanza kutuma nafaka bure.

Haya yanajiri baada ya Urusi kujiondoa katika makubaliano ya Bahari Nyeusi kayi yake na Ukraine mapema mwezi huu.

Putin alisema kuwa Urusi iko tayari kujaza upungufu wowote wa nafaka uliosababishwa na Ukraine.

Aidha ameongeza kuwa Urusi iko tayari kusambaza nafaka kwa nchi sita za Afrika katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo.

Nchi hizo ni Burkina Faso, Zimbabwe, Mali, Somalia, Afrika ya Kati, na Eritrea ambazo zitapokea nafaka bure kutoka Urusi, hazitolipia hata gharama ya usafiri.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya