ZINAZOVUMA:

PACOME aitwa Timu ya Taifa

Pacome aitwa timu ya taifa ya Ivory Coast, baada ya...

Share na:

Mchezaji wa Yanga aliesajiliwa msimu huu kutoka Asec Mimosa maarufu kama Zinedine Zidane wakimfananisha na mchezaji wa zamani wa Ufaransa na Real Madrid. Licha ya kuwa mchezaji bora wa ligi ya Ivory Coast msimu uliopita, bado Pacome alikuwa hawezi kuitwa kwenye kikosi cha taifa. Safari hii nyota imeangukia kwake na ameitwa akachezee timu ya taifa.

Pacome alifanikiwa kuitwa katika wachezaji 50 wa kwanza kwenye kikosi cha Ivory Coast ila hakuweza kupenya kwenye mchujo wa mwisho hata hivyo ilikuwa ni njia ya mafanikio kwenda juu zaidi. Kutokana na mafanikio yake CAF Champions League kwa kuwa mchezaji bora hatua ya makundi, imefungua jicho la kocha wa Ivory Coast kumuona Pacome Zouzua.

The Elephants wanatarajia kucheza tarehe 23 dhidi ya Benin na tarehe 26 dhidi ya Uruguay. Hofu ya mashabiki wa Yanga ni kupata majeraha mechi hizo, kwani ni mchezaji wanayemtegemea kwenye mechi dhidi ya Mamelod Sundowns tarehe 30. Mbali na hofu ya mashabiki wa klabu yake, hii ni hatua kubwa kwa Pacome katika maisha yake ya mpira.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya