Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Real Madrid Mesut Ozil ametangaza kustaafu kucheza mpira wa kulipwa akiwa na umri wa miaka 34.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ozil ameandika na kuwaaga mashabiki wake, klabu mbalimbali alizopita na makocha waliomfundisha akiwashukuru kwa mchango wao katika safari yake ya mpira.
Ozil amesema amefikia hatua hiyo baada ya majeraha ya mara kwa mara hivyo kuona ni muda sahihi sasa wa kupumzika.
Mesut Ozil amecheza kwa mafanikio makubwa sana akiwa Real Madrid pamoja na Arsenal.
Miongoni mwa vilabu alivyopita ni pamoja na Schalke 04, Werder Bremen, Real Madrid, Arsenal, Fernabahce, pamoja na Basaksehir.