ZINAZOVUMA:

“Wanafunzi fanyeni mazoezi”

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ahimiza mazoezi kwa wanafunzi kwa...

Share na:

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka shule zote za msingi na sekondari nchini kuwepo na mazoezi ya viungo kwa wanafunzi ikiwepo kukimbia, mchakamchaka, kutembea na kucheza ngoma au mpira kwa lengo la kupunguza magonjwa yasiyo ambukiza.

Hayo yamesemwa wakati akizindua mkutano wa Kikundi cha Utafiti wa magonjwa ya kisukari na magonjwa yasiyo ambukiza kwa ukanda wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Waziri Ummy amesema lengo la kuzindua kikundi hicho ni kujadili kwa pamoja jinsi ya kuboresha huduma kwa watu wenye ugonjwa wa Kisukari na magonjwa yasiyoambukiza katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Sambamba na hilo, Waziri Ummy amesema kwa sasa nchi ya Tanzania kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na saratani.

Pia, Waziri Ummy amebainisha kuwa Takwimu za mwaka 2012 zinaonesha katika kila watu 100 watu 9 wana ugonjwa wa kisukari ambapo mwaka huu Serikali itafanya tafiti nyingine kwa kuwa inaonekana kuna wagonjwa wengi wa kisukari nchini.


Hata hivyo, Waziri Ummy amesema serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari kwa kuhamasiha ufanyaji wa mazoezi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya