ZINAZOVUMA:

Ombi la Trump lakataliwa

Baada ya ombi la kwanza kukataliwa la kuongezewa muda Donald...

Share na:

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, amesema atawasilisha pingamizi mahakamani, kutaka kesi dhidi yake kuhamishwa kutoka Washington pamoja na jaji anayesikiliza kesi hiyo aondolewe kwa kile anachodau kuwa haoni kama atatendewa haki.

Trump amezidisha mashambulio dhidi ya waendesha mashtaka wanaosimamia kesi yake kuhusu kujaribu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Katika taarifa yake, Trump, amemtuhumu jaji Tanya Chutkan, akisema haamini ikiwa atamtendea haki katika kesi yake, akisisitiza anataka aondolewe au kesi hiyo kuhamishiwa jimbo jingine.

Hatua ya Trump, inakuja baada ya jaji Tanya kutupilia mbali maombi ya mawakili wake kutaka kupewa muda zaidi kujibu hoja za mashtaka, ambapo wanatakiwa kuwasilisha majibu yao baadae hii leo.

Ni jaji Tanya ambaye mwaka 2021, aliamua kesi dhidi ya Trump ambapo alisema rais sio Mfalme.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,