HSBC, benki kubwa zaidi barani Ulaya, imetangaza nia yake ya kuhamisha makao makuu. Benki hiyo inatarajia kuhama kutoka Canary Wharf kwenda katika ofisi ndogo katikati ya mji wa London. Hapo kabla ofisi hizo tarajali zilikuwa zikitumiwa na kampuni ya British telecomunications (BT). jengo hilo lililofanyiwa marekebisho hivi karibuni zinafahamika zaidi kama Panorama St Paul’s.
Uamuzi huu wa kuhamia tathmini iliofanywa na HSBC ili kubainisha eneo bora la baadaye la kuweka benki hiyo jijini London. Benki hiyo imefanya tatmini hiyo hivi karibu ikiwa ni muda mchache kabla ya kuisha mkataba wake katika jengo la sasa. Kwa sasa benki hiyo ina makao makuu yake 8 Canada Square ambapo mkataba utamalizika mwaka 2027.
Chanzo: Reuters